Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Sunday, November 7, 2010

Mwandishi wa Mwananchi aukwaa udiwani pangani

Mwandishi wa Habari anayeaandikia gazeti la Mwananchi wilayani Pangani, John Semkande, ameibuka na ushindi mnono katika kinyang'anyiro cha udiwani kata ya Pangani Magharibi baada ya kumshinda mpinzani wake mkubwa Kitwana Seif wa Chama Cha Wananchi (CUF), Semkande ambaye aligombea kupitia CCM alipata kura 1,126 dhidi ya kura za Kitwana 589.

Akizungumza mara baada ya matokeo hayo Semkande ambaye alimshinda Abdalahaman aliyekuwa makamo mwenyekiti wa halmashauri ya Pangani, alisema kuwa atawatumikia wananchi wa kata hiyo kwa kufuata ilani ya uchaguzi ya CCM waliyoinadi kuondoa kero zilizopokatika kata hiyo.

Alipoulizwa swali la kizushi kwamba kazi yake ya uanishi ataacha au la, Semkande alisema kuwa hawezi kuacha kwani pamoja na kufahamika katika harakati za kuwasaidia watu hata alipokuwa siyo kiongozi, pia kazi hiyo ilimuongezea umaarufu uliomfikisha hapo.

"Nitaandika tu habari hasa za halmashauri kama kutakuwa na wakuu wa idara wanachelewesha ilani yetu ya CCM kwa makusudi nitaandika kufichua ili mambo yaende si unajua kichaa kapewa rungu," alisema mheshimiw adiwani huyo.

No comments:

Post a Comment