MGOMBEA wa ubunge jimbo la Tanga Mjini kupitia Chama Cha mapinduzi (CCM) Injinia Omari Rashid Nundu 'Zindabaa', ametangazwa rasmi kushinda ubunge jimbo hilo kwa kupata kura 40,225 na kuwashinda wagombea wengine wa upinzani waliogombea naye.
Akitangaza matokeo hayo leo hii majira ya saa 8:15 usiku kwenye ofisi za Jiji la Tanga, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo bw. John Maheke Gikene, alisema aliemfuata mgombea huyo ni Mussa Mbaruk wa CUF ambaye amepata kura 24,262, mgombea wa Chadema Kasimu Amari Mbaruk kura 5,750 na Mohamed Mwinyimatano wa UDP aliambulia kura 429.
Gikene alisema jumla ya watu waliojiandikisha kupiga kura ni 179,325 kura halali zilizopigwa ni 72,212 wakati kura 275 ziliharibika.
Akitangaza matokeo ya kura za urais alisema mgombea wa PPT-maendeleo Kuga Mziray amepata kura 306, CCM Jakaya Kikwete amepata kura 42,628, Dkt Willibroad Slaa wa chadema amepata kura 7,353, Prof Ibrahim Lipumba wa CUF amepata kura 20,188, Hashimu Rugwe wa NCCR-mageuzi amepata kura 116, Mutamwega Mugaya wa TLP amepata kura 42 na Dovutwa fahm wa UPDP ameambulia kura 29.
No comments:
Post a Comment