Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa nchini Jack Mugendi Zoka akijitokeza kwa mara ya kwanza mbele ya Waandishi wa Habari nchini, kukanusha taarifa iliyotolewa na mgombea Urais wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt Willbroad Slaa almaarufu 'Mabunduki', kwama idara hiyo imehusika kuchakachua kura za Urais zilizopigwa na wananchi kwa kukipendelea Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho katika matokeo yanayotolewa na tume NEC mgombea wake Dkt Jakaya Kikwete anaongoza hadi sasa.
Zoka aliyemwakilisha Mkurugenzi wa idara hio Rashid Othman ambaye Dkt Slaa ametaka ajiuzulu kwaq kitendeo hicho, alisema kwamba hawahusiki kabisa na matokeo hayo ya kura zilizopigwa na wananchi na kwamba wamemtaka mombea huyo atoe ushahidi unaoonesha kwamba idara hiyo imehusika na 'uchakachuaji' huo wa matokeo hayo ya urais.
Katika tuhuma zake Dkt Slaa alisema anao ushahidi kwamba idara hiyo imehusika na hatua ya 'uchakachuaji' wa kura hizo kutkana na maokeo yanayotanazwa na NEC kuw ahayalingani na yale ambayo yeye kama ,mgombea matokeo aliyokuwa nayo hayalingani na yale yanayotangazwa akitolea mfano na jimbo la Maswa. Blogu hii ya Watu tunasema sisi tunaangalia je wananchi mnasemaje maana chombo hiki huwa hakitoki hadharani je kulikoni? toa maoni yako tuyajadili ukisoma habari hii.
sir,tafadhili naomba kibari kuonana we uso kwa uso, ninayomambokadha, kuhusina masuala ya kiutendaji je? unatambua kuwa mlisha salitiwa wewe,na mkurugenzi mkuu.. zaidi wasilina nime simu 0783078412.
ReplyDelete