MWENYEKITI wa Tume ya Taifa NEC Jaji Lewis Makame, leo alasiri amemtangaza rasmi mgombea wa Chama Cha mapinduzi (CCM) Jakaya Kikwete kuwa mshindi wa kiti cha urais baada ya kupata kura 5,276,827 sawa na asilimia 61.17 ya kura halali zilizopigigwa ambazo ni 8,398,394 sawa na 97.36 akifuatiwa na Dkt Willbroad Slaa wa Chadema ambaye alipata kura 2,271,941 sawa na asilimia 26.34.
Profesa Ibrahim Lipumba ambaye alishukuru kwa niaba ya wagombea wenzake licha ya kutoa ujumbe akiitaka tume ya taifa ya uchaguzi isijivunie matoeo hayo kutokana na idadi ndogo ya watu waliojitokeza kupiga kura na kumkabidhi Rais mteule ilani ya CUF, alipata kura 695,667 sawa na asilimia 8.06, mgombea wa APPT-Maendeleo Kuga mzirai alishika nafasi ya nne kwa kupata kura 96,933 sawa na asilimia 1.12.
Mshindi wa tano alikuwa Hashim Rungwe mgombea wa NCCR-Mageuzi aliyepata kura 26,388 sawa na asilimia 0.31, mgombea wa TLP Mutamwega mugaya alishika nafasi ya sita kwa kupata kura 17,482 sawa na asilimia 0.20 na mgombea wa UPDP Dovutwa Fahm ambaye alitangaza kujitoa alishika mkia kwa kujikusanyia kura 13,176 sawa na asilimia 0.15 ya kura zote halali zilizopigwa.
Katika matokeo hayo watu waliojiandikisha kupiga kura ni 20,137,303 waliopiga kura ni 8,626,283 sawa na asilimia 42.84 na kura zilizoharibika ni 227,803 na kura halali zilikuwa ni 8,398,394 sawa na asilimia 97.36.
No comments:
Post a Comment