Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Friday, December 31, 2010
Thursday, December 30, 2010
MZUNGU ANAPOTEMBELEA AFRIKA
NYASI ZASHIKA VIZURI MKWAKWANI
WATAALAMU WA UWANJA WA MKAKWANI WAKIUKAGUA NAMNA UNAVYOENDELEA KUOTA MAJANI WALIYOYAPANDIKIZA KATIKA UWANJA HUO. |
WATAALAMU HAO WAKIWA NA MENEJA WA UWANJA HUO MBWANA MSUMAI. |
MENEJA WA UWANJA WA MKWAKWANI MBWA MSUMARI AKIWA NA WAGENI WAKE WATAALAMU WA UWANJA HUO. |
WATAALAMU WAKIWA NA WAANDISHI WA HABARI HAWAPO PICHANI BAADA YA KUUKAGUA UWANJA HUO. |
MBUNGE PROFESA MAJIMAREFU ATEMBELEA KITUO CHA AFYA MOMBO KUONA WAGONJWA
HOTELI INAYOUPENDEZESHA MJI WA TANGA NI BOMBA ILE MBAYA.
CHAMA CHA MAALBINO MKOA WA TANGA CHATOA TUNZO KWA VYOMBO VYA HABARI VINAVYOPIGANIA MASLAHI YAO, LIMO MAJIRA.
CUF KWENDA MAHAKAMANI KUPINGA UCHAGUZI WA MEYA TANGA
JAMANI WAANDISHI WA HABARI SI MMEONA NAMNA WALIVYOTUMIA UBABE KUCHAGUA MEYA WENYEWE CCM HUKU KORAM IKIWA HAIJATIMIA, TUTAKWENDA MAHAKAMANI TU KUUPINGA. |
WAZIRI WA UCHUKUZI, OMAR NUNDU AMBAYE NI MBUNGE WA JIMBO LA TANGA AKISALIMIANA NA WAPIGA KURA WAKE NJE YA UKUMBI HUO BAADA YA KAZI YA KUCHAGUA MEYA KUMALIZIKA. |
MKURUGENZI WA JIJI LA TANGA JOHN MAHEKE GIKENE AKIWA AMECHOKA BAADA YA KUFANYA KAZI NGUMU YA KUHAKIKISHA MEYA ANAPATIKANA LICHA YA MADIWANI WA CUF KUKOSEKANA KWENYE UCHAGUZI HUO. |
KUNDI LA WAANDISHI WA HABARI WAKIWA KWENYE OFISI YA MKURUGENZI KUFUATA UFAFANUZI WA NI KWANINI MKURUGENZI HUYO HAKUSOMA MUHUTASARI WA YATOKANAYO NA KIKAO KILICHOVUNJIKA DESEMBA 11 MWAKA HUU. |
Na Mdau Wetu, Tanga.
UCHAGUZI wa Meya na Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Tanga umefanyika Desemba 29 baada ya kuairishwa majuma mawili yaliyopita ukiwa umegubikwa na hila kadhaa ambazo zilikosa majibu kutoka kwa Mkurugenzi wa Jiji hilo John Maheke ambaye ameruhusu kufanyika uchaguzi huo bila kukamilika kwa wajumbe wote.
Tatizo lililojitokeza ni kwa vyama vya CCM na CUF kulalamikiana ambapo CUF wanasema watashiriki mkutano huo endapo jina moja lililozidi kwa CCM litaondolea hatua ambayo ilisababisha askari wa kutuliza ghasia FFU kutanda jingo zima la halmashauri huku wakiwa na mabomu na silaha kuzuia fujo yoyote ile endapo ingetokea.
Katika Uchaguzi huo uliosimamiwa na Mkurugenzi wa Halmashuri ya Jiji la Tanga John Gikene, kabla ya kuanza Daftari la mahudhulio lilipitishwa na madiwani kuandikisha majina yao ili kujua idadi ya wajumbe watakaoshiriki zoezi hilo la kumchagua Meya na naibu wake ambapo Madiwani wote wa CUF waligoma kuandika majina yao kwa madai ya kutaka ufafanuzi wa kikao kilichopita ambacho kilivunjika.
Aidha kwa matiki hiyo madiwani hao 11 wa chama cha wananchi CUF kugoma kujiandikisha, Mkurugenzi alifungua kikao hicho na zoezi la uchaguzi kuanza ambapo kinyume na matarajio yao hawakuruhusiwa kuchagua wala kuchaguliwa kwa mgombea wao kwa kuwa hawakuwa wajumbe wa kiako hicho kwa mujibu wa maelekezo ya msimamizi huyo, hivyo wakabaki kuwa watazamaji tu kama watu wengine waliofika kwenye ukumbi huo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi baada ya uchaguzi huo ulioshirikisha wajumbe 22 wa CCM pekee wakiwemo Waziri wa uchukuzi Omar Nundu na naibu waziri wa Maendeleo ya wanawake na watoto Ummi Ali Mwalimu, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili wa CUF, Omary Mzee ambae ni Diwani wa Kata ya Makorora alisema kuwa hawautambui uchaguzi huo na wanawasiliana na mwanasheria wao ili kuweza kudai haki yao ya kutoshirikishwa katika uchaguzi huo.
Alielezea kuwa uamuzi wa wao kutoshirikishwa kupiga kura ni kinyume na taratibu kwa kuwa kwa mujibu wa katiba wanaostahili kuchagua ni thelusi tatu ya madiwani wote ambao ni sawa na wajumbe 24 katika wajumbe wote 36, ambapo walioshiriki uchaguzi huo ni wajumbe 22 tu.
“Sisi tulitaka kwanza Mkuu atuletee ufafanuzi wa kisheria kutoka tume kwani ndio lengo la kuvunjika kwa kikao cha kwanza, tumefika leo tukaamua kwanza tusisaini hadi tutakapo pewa maelezo…., kisheria wanaopaswa kumchagua meya ni thelusi ya wajumbe sasa huu uchaguzi sisi hatuutambui tunawasiliaana na wanasheria wetu kujua nini tufanye,” alisema Mzee.
Kwa upande wake mgombea aliyesimamishwa na CUF kwa nafasi hiyo ya cha Meya Rashidi Jumbe diwani wa kata ya Mwanzange, alisema Chama tawala kimekuwa natabia ya kupenda kuwa buruza hali iliyosababisha leo kulazimishia uchaguzi na kuufanya kimababe.
“Sisi hatukuja hapa kufanya vurugu tunachofanya ni kuwakilisha mawazo ya wananchi, tumeshangaa kuona askari wameletwa ili kusimamia huu uchaguzi ni dhahiri walijua haki haitatendeka wakajenga hofu, huu uchaguzi umeenda kinyemela,” alisema Jumbe.
Akizungumzia hali hiyo ya wajumbe hao madiwani wa CUF kutoshiriki katika zoezi hilo Mkurugenzi huyo alisema kuwa yeye amejaribu kutumia busara kwani wananchi wanahitaji kuona waliowwachagua wanaanza kazi maramoja na kuhusu madai hayo ya kutotimia wajumbe alisema kuwa yeye ametumia sheria namba nane inayoruhusu nusu ya wajumbe kupitisha maamuzi.
“Nilichofanya ni kufuata busara za kawaida, wangefuta kwanza sheria wajiandikishe halafu waombe ufafanuzi, hatuwezi kuchezea demokrasia kwa itikadi za kisiasa wao walikataa kujiandikisha inamaana hawakua wajumbe na kikao hakiruhusu wasio wajumbe kushiriki uchaguzi maana vikao hivi vinahudhuriwa pia na wananchi,” alisema Gikene na kuongeza
Uchaguzi huo ulimpisha Omari Guledi diwani wa kata ya Ngamiani Kaskazini kwa tiketi ya CCM kuwa meya wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa kura zote za wajumbe 22 na Mzamiru Shemdoe diwani wa kata ya Mabawa CCM kuwa naibu meya aliyekuwa akigombe na Mohamed Mambea wa Kata ya Marungu.
Wednesday, December 29, 2010
MAHAKAMA YAMTIA CHENGE HATIANI, ALIPA FAINI YA 700,000 AACHIWA HURU
Tuesday, December 28, 2010
CHELSEA WASHINDWA KUTAMBA, WABUGIZWA 3-1 NA ARSENAL
WACHEZAJI WA ARSENAL WAKIMPONGEZA KIUNGO WAKE MZUIAJI ALEX SONG BAADA YA KUIANDIKIA TIMU YAKE BAO LA KWANZA KIPINDI CHA PILI KUFUATIA MCHEZAJI HUYO KUCHEZA VIZURI NA ROBIN VAN PERSIE |
CESC FABREGAS AKIPONGEZWA NA MSHABULIZI MWENZAKE WA ARSENAL THEO WALCOTT BAADA YA KUFUNGA BAO LA PILI KWA TIMU YAKE DHIDI YA CHELSEA MCHEZO ULIOFANYIKA KWENYE UWANJA WA EMIRATES. |
ARSENAL IMEKWEA HADI NAFASI YA PILI KATIKA MSIMAMO WA LIGI KUU YA BARCLAYS KUFUATIA MATOKEO YAKE MAZURI YA KUIFUNGA CHELSEA BAO 3-1 KATIKA MCHEZO MKALI ULIOFANIKA KWENYE UWANJA WA EMIRATES MJINI LONDON.
ARSENAL WALIPATA BAO LAO LA KWANZA LILILOFUNGWA NA SONG ALIYEMALIZIA KAZI NZURI ILIYOFANYWA NA VAN PERSIE AMBAYE ALIGONGEANA VIZURI NA MFUNGAJI. BAO HILO LILIDUMU HADI MAPUMZIKO.
KIPINDI CHA PILI KILIPOANZA ARSENAL WALIENDELEA KULISAKAMA LANGO LA CHELSEA AMBAYO HAIKUCHEZA KITIMU KUOKANA NA KUPWAYA SEHEMU YA KIUNGO NA KUSABABISHA WACHEZAJI WA ARSENAL KUTAWALA SEHEMU HIYO ILIYOPELEKEA WAPATE BAO LA PILI LILILOFUNGWA NA FABREGAS ALIYEMALIZIA MPIRA WA KROSI ULIOPIGWA NA MSHAMBULIAJI CHIPUKIZI WALCOTT ALIYEMZIDI MBIO ASHERY COLE NA KUTOA PASI KWA MFUNGAJI.
BAO LA TATU LILIFUNGWA NA WALCOTT AMBAYE ALIANGULIZIWA MPIRA MREFU NA FABREGAS NA KUMTAZAMA KIPA WA CHELSEA PETR CHEC NA KUMFUNGA KIRAHISI.
CHELSEA WALIPATA BAO LAO LA KUFUTIA MACHOZI KUPITIA KWA BEKI WAKE BRANISLAV IVANOVIC ALIYEFUNGA KWA KICHWA KUFUATIA MPIRA WA ADHABU ULIOPIGWA NA DIDIER DROGBAR.
KWA MATOKEO HAYO ARSENAL IMEFIKISHA POINTI 35 DHIDI YA POINTI 37 ZA KINARA WA LIGI HIYO MANCHESTER UNITED AMBAYO IMECHEZA MICHEZO 17 NA ARSENAL MICHEZO 18.
MSIMAMO WA LIGI HIYO NI KAMA IFUATAVYO;
Monday, 27 December 2010 21:59 UK
Position | Team | P | GD | PTS |
---|---|---|---|---|
Full Barclays Premier League table | ||||
1 | Man Utd | 17 | 22 | 37 |
2 | Arsenal | 18 | 17 | 35 |
3 | Man City | 19 | 12 | 35 |
4 | Chelsea | 18 | 17 | 31 |
5 | Tottenham | 18 | 4 | 30 |
6 | Bolton | 19 | 7 | 29 |
7 | Sunderland | 19 | 1 | 27 |
8 | Stoke | 18 | 1 | 24 |
9 | Newcastle | 18 | -1 | 22 |
10 | Liverpool | 17 | -1 | 22 |
11 | Blackpool | 16 | -5 | 22 |
12 | West Brom | 18 | -7 | 22 |
13 | Blackburn | 19 | -7 | 22 |
14 | Everton | 18 | -1 | 21 |
15 | Aston Villa | 18 | -10 | 20 |
16 | Wigan | 18 | -14 | 19 |
17 | Birmingham | 17 | -3 | 18 |
18 | Fulham | 18 | -6 | 16 |
19 | West Ham | 19 | -13 | 16 |
20 | Wolves |
Monday, December 27, 2010
MAN CITY YAIFUNGA ASTON VILLA 2-1 YASHIKA NAFASI YA PILI NYUMA YA MAN UTD
MAN UTD YANG'ANG'ANIA KILELENI, YAIFUNGA SUNDERLAND 2-0, BERBATOV ANGARA TENA
Sunday, December 26, 2010
MTOTO ALIYEZALIWA MUHEZA (BONDE) MKESHA WA CHRISTMASS
BI ELIZABETH GEORGE KUKU AKIWA AMEJIFUNGUA MTOTO WA KIUME KWENYE MKESHA WA SIKUKUU YA CHRISTMASS KATIKA KIJIJI CHA CHA KICHEBA WILAYANI MUHEZA, TANGA. MAMA HUYO NA MTOTO WANAENDELEA VIZURI. |
MTOTO ALIYEZALIWA KWENYE MKESHA WA CHRISTMASS AMBAYE BADO HAJAPEWA JINA LAKINI INAWEZEKANA AKAITWA MOSES. PICHA NA MDAU WETU. |
Saturday, December 25, 2010
HERI YA CHRITSMASS WAPENDWA WETU WOTE
TUNAWATAKIWA KILA KHERI KATIKA SIKUKUU YA CHRISTMASS NA MWAKA MPYA MUNGU AWAJALIE AFYA NJEMA WAPENZI WOTE WA BLOGU HII YA WATU NA MATUKIO, ILA TAADHALI LAZIMA MSHEREHEKEE KWA SALAMA NA AMANI ILI MWAKA HUU UPINDUKE VEMA.
Thursday, December 23, 2010
ISSA MASANINGA NAYE ALIKUWEPO TANGA, SASA HIVI YUPO LINDI
WACHEZAJI COASTAL UNION WAKIJIWINDA DARAJA LA KWANZA 9BORA
KARIBU MGENI WETU BUNGU SEKONDARI
WATOTO TUSIWATENGE TUWAACHE WASOME
Wednesday, December 22, 2010
WANAWAKE WAPENDELEWE KUPATA MAFUNZO ZAIDI YA UKIMWI-SHEIKH LUWUCHU
VIONGOZI WA SERIKALI NA WA TAASISI YA KIISLAMU YA MAAWAL WAKIWA KWENYE SEMINA YA UKIMWI ILIYOFANYIKA KWENYE MOJA YA MAJENGO YA TAASISI HIYO YALIOPO ENEO LA NGAMIANI, MASIWANI. |
WALIMU WA MADRASA MBALIMBALI KUTOKA WILAYA ZA PANGANI, MKINGA NA TANGA MJINI WAKISIKILIZA KWA MAKINI MAWAIDHA YA JUU YA KUENEA KWA VIRUSI VYA UGONJWA WA UKIMWI. |
WALIMU WA MADRASA WAKISIKILIZA SEMINA YA UKIMWI INAYOENDELEA KWENYE TAASISI YA KIISLAMU YA MAAWAL YA JIJINI TANGA, LEO ASUBUHI. |
MASHEIKH WA WILAYA YA PANGANI NA MKINGA WAKISIKILIZA SEMINA HIYO. |
SHEIKH ALI JUMA LUWUCHU SHEIKH WA WILAYA YA PANGANI NA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA BARAZA LA WAISLAMU NCHINI BAKWATA AKITOA NASAHA ZAKE KWENYE SEMINA HIYO. |
HAPA SHEIKH ALI JUMA LUWUCHU AKISITIZA UMUHIMU WA WAUMINI KUANGALIA SUALA LA MAFUNDISHO YA DINI ILI KUEPUKA UGONJWA HUO KAMA AMBAVYO IMEANDIKWA KATIKA KORAN TUKUFU. |
SHEIKH wa wilaya ya Pangani, Sheikh Ali Juma Luwuchu, amesema kuwa ingekuwa bora zaidi kama wanawake wakapendelewa kupewa mafunzo ya elimu juu ya maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI kwa vile akina mama ndiyo walezi wa familia nchini.
Akizungumza leo (jumatano) kwenye semina kwa walimu wa madrasa wa wilaya za Pangani, Mkinga na Tanga mjini iliyoandaliwa na Taasisi ya Kiislamu ya Maawal ya Jijini Tanga, Sheikh Luwuchu alisema kuwa upo umuhimu mkubwa katika jamii katika kutoa mafunzo kwa upendeleo kwa wanawake aliyowaelezea kwamba watakapopatia mafunzo wataweza kusaidia kupungua kwa ugonjwa huo.
Sheikh Luwuchu ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA Taifa, alisema wanaume wanaoshindwa kujizuia na mafundisho ya dini, wamekuwa wakitongoza wanawake na kwenda kufanya zinaa hivyo endapo mwanamke akipata elimu zaidi ya ukimwi ataweza kukataa au kumtaka mwanaume anayemtaka kupima virusi vya ugonjwa huo.
Alisema pia wanawake wakipata mafunzo hayo itasaidia pia kujua namna ya mavazi wanayotakiwa kuvaa ili wasiweze kuvaa yale ambayo yatawashawishi wanaume ambao watapelekea kuwaomba kufanya mapenzi na hatimaye ugonjwa huo kuendelea kusambaa kwa wale waliokwisha ambukizwa.
Naye Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Tanga Dkt Seleman Msangi alisema kuwa bila kuathiri imani ya dini waumini wengi nchini wanatakiwa kufuata mafundisho ya dini zao ili kuepuka vishawishi vya kufanya ngono zembe zitakazosababisha kuenea zaidi kwa maambukizo ya ugonjwa huo.
Dkt huyo aliyekuwa akielelza huku akitoa mifano ya kitabu cha mungu kinachoeleza watu wajikinge hata kabla ya kuwepo kwa ugonjwa huo hatua ambayo aliielezea kwamba endapo waumini watafuata maamrisho hayo ugonjwa huo hauwezi kuenea zaidi na kwamba suala la kujizuia na maambukizi ni la mtu mwenyewe na imani yake ya dini.
"Hata kitabu cha koran kinatutaka tuoe mke mzuri asiyekuwa na mbalanga na ukoma kwa wakati huo kabla ukimwi hakuna leo hii ukoma unatibika lakini maana yake tuoe na kupima ukimwi...Kingine uislamu ukiosha maiti waoshaji walikuwa wakivaa vitambaa na sasa wanavaa glovu hii yote ni kujikinga na maambukizi," alisema Dkt Msaangi.
Mratibu wa semina hiyo iliyofadhiliwa na taasisi ya Civl Foundation, Sheikh Mohamed Hariri alisema kuwa mafunzo hayoa yatasaidia kuwapa uwezo walimu wa madrasa kuuelewa tatizo la ugonjwa huo na kisha kwenda kuwafundisha wanafunzi katika ngazi zao.
Tuesday, December 21, 2010
WAUMINI WA BILAL MUSLIMU WATOA DAMU KUMUENZI IMAMU HUSSEINALIYEUWAWA KWA UPANGA MIAKA 61H
MWINGINE AKIPIMA DAMU KWA MUUGUZI WA HOSPITALI YA BOMBO |
MAKAO MAKUU YA BILAL MUSLIM ILIYOPO BARABARA YA 5 JIJINI TANGA. |
WAKIFANYA MAANDAMANO KUSHEREHEKEA SIKUKUU YAO. |
WAKIENDELEA NA MAANDAMANO KATIKA MITAA MBALIMBALI YA JIJI HILO. |
WANAENDELEA NA MAANDAMANO YAO NA WENGINE WAKIWA KWENYE MAGARI |
NA VIJANA WA AINA MBALIMBALI WALIKUWEPO KWENYE MAANDAMANO HAYO. |
UKIANDAMANA LAZIMA USHIKE KIFUA AU SHINGO NA UONESHE HISIA KWELI |
UTAULIZA HAWAFIKI TU MAANA TANGU HUKO WANAANDAMANA TU LAKINI WALIFIKA KWENYE MSIKITI WAO HUO WA BARABARA 5 WAKAFANYA SHEREHE ZAO HIZO KWA AMANI TU. |
Subscribe to:
Posts (Atom)