VIONGOZI WA SERIKALI NA WA TAASISI YA KIISLAMU YA MAAWAL WAKIWA KWENYE SEMINA YA UKIMWI ILIYOFANYIKA KWENYE MOJA YA MAJENGO YA TAASISI HIYO YALIOPO ENEO LA NGAMIANI, MASIWANI. |
WALIMU WA MADRASA MBALIMBALI KUTOKA WILAYA ZA PANGANI, MKINGA NA TANGA MJINI WAKISIKILIZA KWA MAKINI MAWAIDHA YA JUU YA KUENEA KWA VIRUSI VYA UGONJWA WA UKIMWI. |
WALIMU WA MADRASA WAKISIKILIZA SEMINA YA UKIMWI INAYOENDELEA KWENYE TAASISI YA KIISLAMU YA MAAWAL YA JIJINI TANGA, LEO ASUBUHI. |
MASHEIKH WA WILAYA YA PANGANI NA MKINGA WAKISIKILIZA SEMINA HIYO. |
SHEIKH ALI JUMA LUWUCHU SHEIKH WA WILAYA YA PANGANI NA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA BARAZA LA WAISLAMU NCHINI BAKWATA AKITOA NASAHA ZAKE KWENYE SEMINA HIYO. |
HAPA SHEIKH ALI JUMA LUWUCHU AKISITIZA UMUHIMU WA WAUMINI KUANGALIA SUALA LA MAFUNDISHO YA DINI ILI KUEPUKA UGONJWA HUO KAMA AMBAVYO IMEANDIKWA KATIKA KORAN TUKUFU. |
SHEIKH wa wilaya ya Pangani, Sheikh Ali Juma Luwuchu, amesema kuwa ingekuwa bora zaidi kama wanawake wakapendelewa kupewa mafunzo ya elimu juu ya maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI kwa vile akina mama ndiyo walezi wa familia nchini.
Akizungumza leo (jumatano) kwenye semina kwa walimu wa madrasa wa wilaya za Pangani, Mkinga na Tanga mjini iliyoandaliwa na Taasisi ya Kiislamu ya Maawal ya Jijini Tanga, Sheikh Luwuchu alisema kuwa upo umuhimu mkubwa katika jamii katika kutoa mafunzo kwa upendeleo kwa wanawake aliyowaelezea kwamba watakapopatia mafunzo wataweza kusaidia kupungua kwa ugonjwa huo.
Sheikh Luwuchu ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA Taifa, alisema wanaume wanaoshindwa kujizuia na mafundisho ya dini, wamekuwa wakitongoza wanawake na kwenda kufanya zinaa hivyo endapo mwanamke akipata elimu zaidi ya ukimwi ataweza kukataa au kumtaka mwanaume anayemtaka kupima virusi vya ugonjwa huo.
Alisema pia wanawake wakipata mafunzo hayo itasaidia pia kujua namna ya mavazi wanayotakiwa kuvaa ili wasiweze kuvaa yale ambayo yatawashawishi wanaume ambao watapelekea kuwaomba kufanya mapenzi na hatimaye ugonjwa huo kuendelea kusambaa kwa wale waliokwisha ambukizwa.
Naye Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Tanga Dkt Seleman Msangi alisema kuwa bila kuathiri imani ya dini waumini wengi nchini wanatakiwa kufuata mafundisho ya dini zao ili kuepuka vishawishi vya kufanya ngono zembe zitakazosababisha kuenea zaidi kwa maambukizo ya ugonjwa huo.
Dkt huyo aliyekuwa akielelza huku akitoa mifano ya kitabu cha mungu kinachoeleza watu wajikinge hata kabla ya kuwepo kwa ugonjwa huo hatua ambayo aliielezea kwamba endapo waumini watafuata maamrisho hayo ugonjwa huo hauwezi kuenea zaidi na kwamba suala la kujizuia na maambukizi ni la mtu mwenyewe na imani yake ya dini.
"Hata kitabu cha koran kinatutaka tuoe mke mzuri asiyekuwa na mbalanga na ukoma kwa wakati huo kabla ukimwi hakuna leo hii ukoma unatibika lakini maana yake tuoe na kupima ukimwi...Kingine uislamu ukiosha maiti waoshaji walikuwa wakivaa vitambaa na sasa wanavaa glovu hii yote ni kujikinga na maambukizi," alisema Dkt Msaangi.
Mratibu wa semina hiyo iliyofadhiliwa na taasisi ya Civl Foundation, Sheikh Mohamed Hariri alisema kuwa mafunzo hayoa yatasaidia kuwapa uwezo walimu wa madrasa kuuelewa tatizo la ugonjwa huo na kisha kwenda kuwafundisha wanafunzi katika ngazi zao.
No comments:
Post a Comment