Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Thursday, December 30, 2010

CUF KWENDA MAHAKAMANI KUPINGA UCHAGUZI WA MEYA TANGA


MADIWANI WA CUF WAKITOKA KATIKA UKUMBI WA WA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA ALIYEKUMBATIWA NI MUSSA MBAROUK ALIYEONGOZA WENZAKE KUSUSIA TENA KIKAO KWA KUKAA KIMYA BILA KUJIANDIKISHA KWENYE KITABU CHA MAHUDHURIO.

ALIYEKUWA MGOMBEA UMEYA WA JIJI LA TANGA KUPITIA CHAMA CHA WANANCHI CUF, RASHID JUMBE AMBAYE NI DIWANI WA CHAMA HICHO KATIKA KATA YA MWANZANGE, AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUTOA MSIMAMO WAKE WA KWENDA MAHAKAMANI BAADA YA KUTORIDHISHWA NA HATUA YA KUVURUGWA TENA UCHAGUZI HUO.


JAMANI WAANDISHI WA HABARI SI MMEONA NAMNA WALIVYOTUMIA UBABE KUCHAGUA MEYA WENYEWE CCM HUKU KORAM IKIWA HAIJATIMIA, TUTAKWENDA MAHAKAMANI TU KUUPINGA.

WAZIRI WA UCHUKUZI, OMAR NUNDU AMBAYE NI MBUNGE WA JIMBO LA TANGA AKISALIMIANA NA WAPIGA KURA WAKE NJE YA UKUMBI HUO BAADA YA KAZI YA KUCHAGUA MEYA KUMALIZIKA.


MEYA WA JIJI LA TANGA OMAR GULED AMBAYE NI DIWANI WA KATA YA NGAMIANI KASKAZINI AKITETA NA NAIBU WAKE MUZAMIN SHEMDOE DIWANI WA KATA YA MABAWA MUDA MFUPI BAADA YA KUCHAGULIWA NAFASI HIZO. HAPA WAKIWA OFISI KWA MEYA WAKIPANGA MAJINA YA WAJUMBE WA KAMATI MBALIMBALI ZA HALMASHAURI HIYO.

MKURUGENZI WA JIJI LA TANGA JOHN MAHEKE GIKENE AKIWA AMECHOKA BAADA YA KUFANYA KAZI NGUMU YA KUHAKIKISHA MEYA ANAPATIKANA LICHA YA MADIWANI WA CUF KUKOSEKANA KWENYE UCHAGUZI HUO.


KUNDI LA WAANDISHI WA HABARI WAKIWA KWENYE OFISI YA MKURUGENZI KUFUATA UFAFANUZI WA NI KWANINI MKURUGENZI HUYO HAKUSOMA MUHUTASARI WA YATOKANAYO NA KIKAO KILICHOVUNJIKA DESEMBA 11 MWAKA HUU.

Na Mdau Wetu, Tanga.
UCHAGUZI wa Meya na Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Tanga umefanyika Desemba 29 baada ya kuairishwa majuma mawili yaliyopita ukiwa umegubikwa na hila kadhaa ambazo zilikosa majibu kutoka kwa Mkurugenzi wa Jiji hilo John Maheke ambaye ameruhusu kufanyika uchaguzi huo bila kukamilika kwa wajumbe wote.

Tatizo lililojitokeza ni kwa vyama vya CCM na CUF kulalamikiana ambapo CUF wanasema watashiriki mkutano huo endapo jina moja lililozidi kwa CCM litaondolea hatua ambayo ilisababisha askari wa kutuliza ghasia FFU kutanda jingo zima la halmashauri huku wakiwa na mabomu na silaha kuzuia fujo yoyote ile endapo ingetokea.

Katika Uchaguzi huo uliosimamiwa na Mkurugenzi wa Halmashuri ya Jiji la Tanga John Gikene, kabla ya kuanza Daftari la mahudhulio lilipitishwa na madiwani kuandikisha majina yao ili kujua idadi ya wajumbe watakaoshiriki zoezi hilo la kumchagua Meya na naibu wake ambapo Madiwani wote wa CUF waligoma kuandika majina yao kwa madai ya kutaka ufafanuzi wa kikao kilichopita ambacho kilivunjika.

Aidha kwa matiki hiyo madiwani hao 11 wa chama cha wananchi CUF kugoma kujiandikisha, Mkurugenzi alifungua kikao hicho na zoezi la uchaguzi kuanza ambapo kinyume na matarajio yao hawakuruhusiwa kuchagua wala kuchaguliwa kwa mgombea wao kwa kuwa hawakuwa wajumbe wa kiako hicho kwa mujibu wa maelekezo ya msimamizi huyo, hivyo wakabaki kuwa watazamaji tu kama watu wengine waliofika kwenye ukumbi huo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi baada ya uchaguzi huo ulioshirikisha wajumbe 22 wa CCM pekee wakiwemo Waziri wa uchukuzi Omar Nundu na naibu waziri wa Maendeleo ya wanawake na watoto Ummi Ali Mwalimu, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili wa CUF, Omary Mzee ambae ni Diwani wa Kata ya Makorora alisema kuwa hawautambui uchaguzi huo na wanawasiliana na mwanasheria wao ili kuweza kudai haki yao ya kutoshirikishwa katika uchaguzi huo.

Alielezea kuwa uamuzi wa wao kutoshirikishwa kupiga kura ni kinyume na taratibu kwa kuwa kwa mujibu wa katiba wanaostahili kuchagua ni thelusi tatu ya madiwani wote ambao ni sawa na wajumbe 24 katika wajumbe wote 36, ambapo walioshiriki uchaguzi huo ni wajumbe 22 tu.

“Sisi tulitaka kwanza Mkuu atuletee ufafanuzi wa kisheria kutoka tume kwani ndio lengo la kuvunjika kwa kikao cha kwanza, tumefika leo tukaamua kwanza tusisaini hadi tutakapo pewa maelezo…., kisheria wanaopaswa kumchagua meya ni thelusi ya wajumbe sasa huu uchaguzi sisi hatuutambui tunawasiliaana na wanasheria wetu kujua nini tufanye,” alisema Mzee.

Kwa upande wake mgombea aliyesimamishwa na CUF kwa nafasi hiyo ya cha Meya Rashidi Jumbe diwani wa kata ya Mwanzange, alisema Chama tawala kimekuwa natabia ya kupenda kuwa buruza hali iliyosababisha leo kulazimishia uchaguzi na kuufanya kimababe.

“Sisi hatukuja hapa kufanya vurugu tunachofanya ni kuwakilisha mawazo ya wananchi, tumeshangaa kuona askari wameletwa ili kusimamia huu uchaguzi ni dhahiri walijua haki haitatendeka wakajenga hofu, huu uchaguzi umeenda kinyemela,” alisema Jumbe. 

Akizungumzia hali hiyo ya wajumbe hao madiwani wa CUF kutoshiriki katika zoezi hilo Mkurugenzi huyo alisema kuwa yeye amejaribu kutumia busara kwani wananchi wanahitaji kuona waliowwachagua wanaanza kazi maramoja na kuhusu madai hayo ya kutotimia wajumbe alisema kuwa yeye ametumia sheria namba nane inayoruhusu nusu ya wajumbe kupitisha maamuzi.

“Nilichofanya ni kufuata busara za kawaida, wangefuta kwanza sheria wajiandikishe halafu waombe ufafanuzi, hatuwezi kuchezea demokrasia kwa itikadi za kisiasa wao walikataa kujiandikisha inamaana hawakua wajumbe na kikao hakiruhusu wasio wajumbe kushiriki uchaguzi maana vikao hivi vinahudhuriwa pia na wananchi,” alisema Gikene na kuongeza

Uchaguzi huo ulimpisha Omari Guledi diwani wa kata ya Ngamiani Kaskazini kwa tiketi ya CCM kuwa meya wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa kura zote za wajumbe 22 na Mzamiru Shemdoe diwani wa kata ya Mabawa CCM kuwa naibu meya aliyekuwa akigombe na Mohamed Mambea wa Kata ya Marungu.

No comments:

Post a Comment