WACHEZAJI WA ARSENAL WAKIMPONGEZA KIUNGO WAKE MZUIAJI ALEX SONG BAADA YA KUIANDIKIA TIMU YAKE BAO LA KWANZA KIPINDI CHA PILI KUFUATIA MCHEZAJI HUYO KUCHEZA VIZURI NA ROBIN VAN PERSIE |
CESC FABREGAS AKIPONGEZWA NA MSHABULIZI MWENZAKE WA ARSENAL THEO WALCOTT BAADA YA KUFUNGA BAO LA PILI KWA TIMU YAKE DHIDI YA CHELSEA MCHEZO ULIOFANYIKA KWENYE UWANJA WA EMIRATES. |
ARSENAL IMEKWEA HADI NAFASI YA PILI KATIKA MSIMAMO WA LIGI KUU YA BARCLAYS KUFUATIA MATOKEO YAKE MAZURI YA KUIFUNGA CHELSEA BAO 3-1 KATIKA MCHEZO MKALI ULIOFANIKA KWENYE UWANJA WA EMIRATES MJINI LONDON.
ARSENAL WALIPATA BAO LAO LA KWANZA LILILOFUNGWA NA SONG ALIYEMALIZIA KAZI NZURI ILIYOFANYWA NA VAN PERSIE AMBAYE ALIGONGEANA VIZURI NA MFUNGAJI. BAO HILO LILIDUMU HADI MAPUMZIKO.
KIPINDI CHA PILI KILIPOANZA ARSENAL WALIENDELEA KULISAKAMA LANGO LA CHELSEA AMBAYO HAIKUCHEZA KITIMU KUOKANA NA KUPWAYA SEHEMU YA KIUNGO NA KUSABABISHA WACHEZAJI WA ARSENAL KUTAWALA SEHEMU HIYO ILIYOPELEKEA WAPATE BAO LA PILI LILILOFUNGWA NA FABREGAS ALIYEMALIZIA MPIRA WA KROSI ULIOPIGWA NA MSHAMBULIAJI CHIPUKIZI WALCOTT ALIYEMZIDI MBIO ASHERY COLE NA KUTOA PASI KWA MFUNGAJI.
BAO LA TATU LILIFUNGWA NA WALCOTT AMBAYE ALIANGULIZIWA MPIRA MREFU NA FABREGAS NA KUMTAZAMA KIPA WA CHELSEA PETR CHEC NA KUMFUNGA KIRAHISI.
CHELSEA WALIPATA BAO LAO LA KUFUTIA MACHOZI KUPITIA KWA BEKI WAKE BRANISLAV IVANOVIC ALIYEFUNGA KWA KICHWA KUFUATIA MPIRA WA ADHABU ULIOPIGWA NA DIDIER DROGBAR.
KWA MATOKEO HAYO ARSENAL IMEFIKISHA POINTI 35 DHIDI YA POINTI 37 ZA KINARA WA LIGI HIYO MANCHESTER UNITED AMBAYO IMECHEZA MICHEZO 17 NA ARSENAL MICHEZO 18.
MSIMAMO WA LIGI HIYO NI KAMA IFUATAVYO;
Position | Team | P | GD | PTS |
---|---|---|---|---|
Full Barclays Premier League table | ||||
1 | Man Utd | 17 | 22 | 37 |
2 | Arsenal | 18 | 17 | 35 |
3 | Man City | 19 | 12 | 35 |
4 | Chelsea | 18 | 17 | 31 |
5 | Tottenham | 18 | 4 | 30 |
6 | Bolton | 19 | 7 | 29 |
7 | Sunderland | 19 | 1 | 27 |
8 | Stoke | 18 | 1 | 24 |
9 | Newcastle | 18 | -1 | 22 |
10 | Liverpool | 17 | -1 | 22 |
11 | Blackpool | 16 | -5 | 22 |
12 | West Brom | 18 | -7 | 22 |
13 | Blackburn | 19 | -7 | 22 |
14 | Everton | 18 | -1 | 21 |
15 | Aston Villa | 18 | -10 | 20 |
16 | Wigan | 18 | -14 | 19 |
17 | Birmingham | 17 | -3 | 18 |
18 | Fulham | 18 | -6 | 16 |
19 | West Ham | 19 | -13 | 16 |
20 | Wolves |
No comments:
Post a Comment