Mchezaji wa Arsenal Jack Wilshere akipimana ubavu na beki wa CS Braga Luis Aguiar katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa uliofanyika nchini Ureno wenyeji waloshinda 2-0 |
Mshambuliaji huyo alipata mpira mrefu dakika saba kabla ya mpira huo kumalizika na kumchambua kipa wa Arsenal Lukasz Fabianski, goli jingine Matheus alifunga katika muda wa majeruhi akitumia makosa ya mabeki kumuacha kufuatia mpira mrefu uliopigwa na beki wa Braga Echiejile na mshambuliaji huyo kuukwamishwa wavuni mpira huo uliopiga juu ya mlingoti kabla ya kutinga wavuni.
Arsenal ilielekea kupata penalt wakati matokeo yakiwa 0-0, lakini Carlos Vela alipewa kadi ya njano na mwamuzi V. Kassai wa Uswisi ambaye alikataa penalti hiyo na kumpa kadi akidai amejiangusha kusudi kwa kuruka kabla ya mpira kumfikia beki wa Braga.
Kikosi hicho cha Gunners pia ilbidi nahodha wake Cesc Fabregas kuomba kutoka nje na nafasi yake kuchukuliwa na Mfaransa Samir Nassir na baadaye Emanuel Eboue alitoka nje baada ya kuumia na timu hiyo ilikuwa tayari imemaliza kuingiza wachezaji watatu na hivyo ikacheza ikiwa na pengo la beki huyo.
Michezo mingine Chelsea ilitoka nyuma na kushinda bao 2-1 dhidi ya Zelin
Arsenal itabidi wamsajili tena Henry, Pires na Lumbgue.....
ReplyDelete