Kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki Duniani, Papa Benedict xvi ametangaza rasmi kuundwa kwa jimbo jipya la katoliki la Bunda na Ukerewe. Jimbo la Bunda na Ukerewe linaundwa kutokana na vipande vya jimbo la Mwanza na Musoma. Katika hatua nyingine Papa amemteua Padre Renatus Nkwande kuwa Askofu wa jimbo hilo jipya.
Askofu mpya mteule huyo Nkwande ndoa yake ya mwisho kuifungisha ilikuwa ni Novemba 6 mwaka huu mjini Mwanza katika kanisa Katoliki la Bugando alipofungisha ndoa baina ya Bw. Joseph Sura na Mama Calvin ndoa ambayo aliibariki na kuwa ya mwisho hadi kuteuliwa kuwa Askofu nafasi ambayo ni kubwa. Mungu ambariki askofu huyo mpya.
|
No comments:
Post a Comment