Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Tuesday, November 23, 2010

JIJI LA TANGA NI SHAMBA LA BIBI...MIL 17 ZATAFUNWA

  Bw. Selemani Mofia Mjumbe wa kikundi cha Chumvini-Kisosora Ngome                                         

Wana-Kikundi walia kutapeliwa Mil. 17 za ununuzi hewa wa boti

*Walipewa fedha na serikali lakini viongozi wametapeli
*Viongozi wawakana wajumbe wa kikundi
*TASAF waliotoa fedha wasikia utapeli lakini hawajui wafanyeje
                                                               
                     Na Mashaka Mhando,Tanga
WANA-kikundi cha uvuvi kilichopo eneo la Ngome-Kisosora katika Jiji la Tanga, wameulalamikia uongozi wao kwa kutokuwa wakweli juu ya matumizi ya fedha kiasi cha shilingi milioni 17 zilizotolewa na serikali kupitia mradi wa Uvuvi na Uhifadhi wa Mazingira katika Mwambao wa Pwani (MACEMP) kwa ajili ya kununulia boti na mashine ya kisasa ya uvuvi.

Wakizungumza jana na gazeti hili, baadhi ya wana-kikundi hao, walisema kuwa serikali iliwapa kwa awamu mbili kiasi cha shilingi milioni 17 kwa ajili ya kununulia boti na mashine yake fedha ambazo zilitolewa kupitia Mradi wa Maendeleo ya Wananchi (TASAF), lakini fedha hizo tangu zitolewe hakuna boti wala mashine iliyonunuliwa na viongozi wao Mwenyekiti na Katibu wa kikundi hicho, hawajawapa taarifa za kuwepo kwa boti hiyo.

Bw. Selemani Mofia alisema sababu ya kufika kwenye vyombo ya habari kulalamikia hali hiyo ni kauli iliyotolewa na viongozi hao kwamba wanataka kuandika barua kuipeleka polisi na TASAF kuelezea kwamba boti imezama baharini na kwamba kikundi hicho hakina tena msaada wa serikali hivyo waandaliwe fedha nyingine ili kununua boti nyingine.

Akifafanua zaidi Bw. Mofia aliyeongozana na Mwekahazina wa kikundi hicho Bi Mwanahawa George, alisema tangu mchakato wa kutolewa fedha hizo, Mwenyeikiti Bw. Faki Heri na Katibu Bw. Hamisi Bonye, walikuwa wakifuatilia fedha hizo lakini hawakuwa wakitoa taarifa kwewnye kikundi juu ya kupatikana fedha hizo na walipowahoji, walisema fedha zimetoka na zote wamempa diwani kwa ajili ya kununua boti na mashine yake.

Alisema katikati ya mwaka huu, wakaguzi wa TASAF na MACEMP walifika kutaka kukagua mradi huo lakini cha kushangaza kabla wakaguzi hao hawajafika walipigiwa simu na mratibu wa TASAF Bw. Ramadhan Posi kwamba, wakaguzi wanakuja na ndipo walipomuona mwenyekiti wao, akipaka rangi moja ya boti zake anazomiliki ambayo wakaguzi hao walioneshwa kwamba ndiyo iliyonunuliwa kwa shilingi milioni 17.

"Tulishangaa sana tulipowauliza baadaye wakasema walifanya vile ili kuonesha kwamba boti tunayo lakini wakasisitiza kwamba boti bado haijanunuliwa akatutaka tuvute subira...Sasa hatujui kuna mchezo gani unafanyika hapa unajua hizi fedha zinaonesha zimeliwa na viongozi wetu wakishirikiana na watendaji wa Jiji kwasababu tumegundua kumbe hata risiti za manunuzi wanazo lakini wana-kikundi sisi hatuoneshwi boti yetu iko wapi," alisema Bw. Mofia kwa masikitiko makubwa.

Alisema kali zaidi hivi juzi juzi mwenyekiti wao aliwafata na kuwaeleza kwamba kikundi kiandike barua kuipeleka polisi kuelelza kwamba boti imepotea baharini ili jeshi hilo liweze kuweka kumbukumbu ya mradi huo kupoteza boti yake hata ambayo aliielezea kwamba kama utapeli mkubwa unafanywa kuhalalisha upotevu wa fedha za serikali zilizotolewa kwa malengo ya kuwasaidia wananchi wake.

Akizungumzia madai hayo Mweneykiti wa Kikundi hicho Bw. Faki aliwakana wanakikundi hao waliozungumza na gazeti hili akidai kwamba hao siyo wanachama wake ingawa alipomuonesha mwandishi wa habari hizi leja yenye majina waliyoandika kupeleka TASAF kwa ajili ya kupewa fedha hizo, majina ya wanakikundi hao yalikuwepo na jina la mwekahazina Bi Mwanahawa limewekwa kama mjumbe na Mwekahazina ni Bw.Filipo Jenzi.

"Unajua hao waliokuja kwako siyo wanakikundi na jingine eneo lile la Ngome kumekuwepo na ukabila lipo suala la Upemba na Utanga...Sasa wanaona kwanini sisi tupate fedha hizi mbona wao hawasemi wamepewa zaidi ya milioni 20 na serikali kwa ajili ya ujenzi wa bwawa lakini wamekula wanaona hizi milioni 17 ambazo ni kidogo tofauti na zao," alisema Bw. Faki na kushindwa kujibu kama boti ipo au haipo ingawa alionesha risiti za fedha wanazoingiza benki zinazopatikana kwenye kikundi hicho.

Mratibu wa TASAF Jiji la Tanga Bw. Posi, alipoulizwa kuhusu malalamiko hayo, alikiri kusikia kwamba kuna usanii umefanyika juu ya ununuzi wa boti hilo lakini wao wameshindwa kugundua kwa kuwa viongozi hao wamewaonesha risiti za kununua boti hiyo na kwamba hawajui wafanyeje ngawa pia alikiri kwamba wananchi wa Jiji la Tanga, hawana ukweli katika matuminzi ya fedha za serikali.

"Mimi nimesikia suala la utapeli kwamba boti halijanunuliwa lakini wale viongozi wametuonesha risiti na tulipokwenda kukagua boti walituonesha...Kwa kweli kufaya kazi na watu wa Tanga ni ngumu mno miradi mingi imekuwa na matatizo ya upotevu wa fedha bure," alisema Bw. posi.

No comments:

Post a Comment