Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Tuesday, November 23, 2010

MBIO ZA UMEYA JIJI LA TANGA ZAINGIA UDINI


Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Tanga Bi Mariam Shamte mtangazaji wa zamani wa BBC

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Bw. Gustav Muba
Umeya Tanga kizungumkuti udini watawala

*Wagombea wanuka tuhuma nzito
*Wanaofaa waambiwa ni Wakristo
*Wanaharakati wasema mbona Mwakitwange alikuwa Meya na ni Mkristu                                         
                           

                        Na Mwandishi Wetu,Tanga
MBIO za kusaka Meya wa Jiji la Tanga, linazidi kupamba moto huku kukiwa na taarifa za baadhi ya wagombea waliochukua fomu za kuwania kiti hicho, kuchafuliwa kwa kuibuliwa tuhuma walizokuwa nazo wakiwa watumishi wa serikali kabla ya kuingia kwenye udiwani na wengine wakiandamwa na mzimu wa dini zao.

Duru za kisiasa za Jiji hilo zinasema kwamba kati ya wagombea saba waliochukua fomu za kugombea kiti hicho, wanaelezwa kwamba hawatoshi kushika nafasi hizo kutokana na mambo mbalimbali waliyofanya wakiwa watumishi wa serikali na wengine wanaoonekana kuwa safi kuchafuliwa kutokana na dini aliyokuwa nayo mgombea huyo.

Katibu wa CCM wilaya ya Tanga Bw. Shekue Pashua aliwataja waliochukua fomu kata zao zikiwa kwenye mabano ni pamoja na Bw. Omar Guled (Ngamiani Kaskazini), Bw. Danny Mgaza (Mzizima), Bw. Muhina Mustafa 'Seleboss' (Nguvumali), Bw. Abdi Abu (Tangasisi), Bw. Fadhil Bwanga (Mzingani), Bw. Telesphor Chambo (Chumbageni) na Bi Mwana-Uzia Juma wa kata ya Pongwe. Wakati Muzamil Shemdoe (Mabawa) na George Mayala (Kiomoni) wameomba Unaibu Meya na Rukia Mapinda na Saida Ghadaf (Viti Maalum) wameomba Ukatibu wa madiwani.

Habari za kichunguzi zilizopatikana kutoka vyanzo mbalimbali vya habari wakiwemo baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Siasa ya wilaya ya Tanga, zinasema wagombea mbalimbali walioomba kiti hicho wakati wakijadiliwa na kamati hizo kulikuwa na taaifa zilizowasilishwa kwenye kikao hicho zikionesha tuhuma mbalimbali za baadhi ya wagombea hao huku hoja ya udini pia ilichukua nafasi kwa baadhi ya wagombea hao.

"Wamejadiliwa na majina yao yamepewa alama kulingana na sifa zao, lakini sisi wajumbe tumekuta karatasi zenye taarifa mbalimbali za tuhuma za wagombea wote walioomba, kwa kweli wapo wenye tuhuma nzito ambazo kama Chama itabidi zizingatiwe unajua wengine hawakuonesha uaminifu huko walikotoka serikalini," alisema mjumbe mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, Karatasi zenye tuhuma hizo MZEE WA BONDE anazo nakala zake zilizochapwa kwenye kompyuta zikiwa na majina ya wagombea wote ingawa wengine tuhuma zao ni kuungwa mkono na baadhi ya viongozi wa CCM ambao hawakubaliki na wameangushwa kwenye nafasi zao.

Mjumbe mwingine alisema kuwa yupo mjumbe kwenye kikao chao wakati wa kujadili majina hayo aliwasilisha hoja ya suala la udini kwamba Meya wa Jiji hilo anatakiwa kuwa Muislamu kutokana na historia ya wakazi wa Tanga na Jiji hilo halikuwahi kuwa na Meya wa dini hiyo, hatua ambayo ilizingatiwa ingawa baadhi ya wajumbe walipinga hoja hiyo wakieleza kwamba kinachotakiwa ni kupata Meya mwenye uwezo, uadilifu na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM ikiwemo miongozo ya serikali za Mitaaa (TAMISEMI).

Akizungumzia suala hilo, Katibu wa CCM wilaya ya Tanga, Bw. Pashua alionesha kushangaa taarifa hizo na kueleza kwamba katika wagombea hao Wakristo wapo wawili na wamepewa alama nzuri tu za mapendekezo za sifa za kustahili kuwa Meya na kwamba majina yote ya wagombea hao tayari wameyawasilisha katika ngazi ya mkoa kwa ajili ya hatua zaidi kwa kuwa kikao chao hakina mamlaka ya kuteua Meya na kueleza suala la jinsi tu lilijitokeza kwa vile yupo diwani mmoja mteule mwanamke amejitokeza kuomba nafasi hiyo.

"Katika wagombea wote saba pale Wakristo ni wawili tena wamepewa alama nzuri tu katika mapendekezo yetu kwa vile wana sifa na haki yao ya kisheria na kikatiba ya kugombea nafasi hiyo, isipokuwa labda kulijitokeza suala la jinsi unajua kuna mwanamke mmoja amegombea na sisi kule Dodoma tulisisitizwa tuwape nafasi pia wanawake wenye uwezo kuwania nafasi hiyo," alisema Bw. Pashua na kupinga suala la udini.

Hadi jana usiku kikao cha Kamati ya Siasa ya mkoa wa Tanga chini ya Mwenyekiti wake Bw. Mussa Shekimweri kilikuwa kikiendelea kuchuja majina ya wagombea hao na wale walioomba nafasi za U-enyekiti wa halmashauri nyingine nane zilizopo mkoani humo kisha baadaye watapelekaq majina matatu katika Kamati Kuu ya CCM kwa ajili ya kuteua jina moja litakalopigiwa kura na madiwani wengine.

Baadhi ya wanaharakati katika Jiji la Tanga, wameelezea kwamba safari hii wanamtaka Meya muadilifu ambaye ataivusha halmashauri hiyo na kuirudisha imani serikali kutokana na watangulizi waliopita kuiharibu ikiwemo kuwapa makandarasi zabuni ambao baadhi yao hawakuwa na uwezo hivyo barabara zinazotengewa fedha nyingi kuharibika katika kipindi kifupi hasa suala la taa za barabarani mradi ambao hadi leo ni ktendawili kilichokosa kuteguliwa.

Wanaharakati hao, walisema kuwa miaka ya nyuma alikuwepo meya aliyeitwa Mzee Mwakitwange ambaye alikuwa ni Mkristu lakini aliweza kuleta maendeleo hadi leo vipo vitu ambavyo vinakumbukwa katika Jiji hilo kama Kituo Kikuu cha mabasi Soko la Ngamiani na mambo mengine lakini mameya waliopita hawana chochote walichofanya zaidi ya kuwapa makandarasi feki ambao wameharibu barabara.

No comments:

Post a Comment