Bi Sekela Mwambali wa Water Aid (kushoo) akifanya mahojiano na Mtangazaji wa Breeze FM, Betha Mwambela kwenye banda la Wate Aid Tangamano.
Mkuu wa wilaya ya Tanga, Dkt. Ibrahim Msengi alipotembelea banda la Water Aid hapa akipewa maneno machache ya kazi zinazofanywa na Bi Sekela Mwambali.
Bi Sekela Mwambali akimweleza Dkt Ibrahim Msengi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Tanga, kwamba shughuli zao zinaambatana na usafi wa mazingira na matumizi ya vyoo bora kwa kuhakisha maji safi yanapatikana.
Mkuu wa wilaya ya Tanga Dkt Ibrahim Msengi (aliyeshika kitambaa cheupe) na Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Paul Amaniel Chikira (kushoto kwa DC), wakiangalia mfano wa namna vyoo vinavyochimbwa katika wilaya ya pangani kwenye banda la wilaya hiyo, choo hicho kimetengenezwa na makumbi ya nazi.
Mkuu wa wilaya Dkt Ibrahim msengi ambaye alifungua sherehe za maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira, siku ya kunawa mikono na siku ya matumizi ya choo duniani Kitaifa iliyofanyika Mkoani Tanga katika Jiji la Tanga.
Wadau mbalimbali kutoka wilaya za mkoa wa Tanga, walihudhuria sherehe hizo wakiwemo vikosi vya ulinzi na usalama.
Maji vipi yanapatikana lakini? ndivyo alivyowauliza wafanyakazi wa mamlaka ya majisai na majitaka alipofika kwenye banda la mamlaka hiyo Tanga-Uwasa.
Hapa tunatoa huduma za UKIMWI!!!!!! ndivyo mhudumu huyu wa TAWUG asasi inayotoa huduma za magojwa ya Ukimwi mkoani Tanga nao hawakubaki nyuma katika sherehe hizo.
No comments:
Post a Comment