Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Saturday, November 20, 2010

WARAKA MTIZAMO KABLA JK HAJAWASILISHA JINA LA MIZENGO PINDA KUWA WAZIRI MKUU....USOME TOA MAONI.

Waraka huu uliandikwa kabla rais Jakaya Kikwete hajawasilisha jina la Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda hajateuliwa kwa mara nyingine tena kwenye nafasi hiyo...usome kwa makini ujue dhana nzima iliyogubika hapa.
WABUNGE kadhaa zikiwemo sura mpya zilizoingia bungeni kwa mara ya kwanza, wanatajwa kuupata uwaziri katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete kwa muhula wake wa mwisho wa 2010-2015, baraza hilo linatarajiwa kutajwa wakati wowote wiki hii akianzia kuteua jina la Waziri Mkuu litakalothibitishwa kesho na bunge la Jamhuri ya muungano.
Waziri Mkuu huyo ambaye anatakiwa kuwa ni mchapakazi hasa kutokana na ahadi lukuki ambazo zimeaanishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM na zile za papo kwa papo alizotoa mwenyewe Rais, baada ya kuteuliwa na rais ataweza kushauriana naye namna ya kupata mawaziri watakaosaidia kusukuma ilani hiyo ili kuhakikisha kivuli cha miaka hii mitano hakiisumbui CCM 2015.
Waziri Mkuu anayetakiwa kuteuliwa ni yule ambaye ana uwezo na sifa ya ya kuwasimamia mawaziri wengine bila woga na kuwaongoza katika kumsaidia Rais Kikwete ili aweze kutimiza kasi, ari na nguvu zaidi katika kuhakikisha utekelezaji wa ahadi zilizoahidiwa zinatekelezwa kwa kiwango kikubwa kile ili kuivusha CCM na ujazi ujao.
Wakati tukiangalia Waziri Mkuu ni vema serikali itakayoundwa Rais akazingatia ukubwa wa baraza lake kutokana na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa kuleza kwamba unapokuwa na baraza dogo utaweza  kupunguza gharama za uendeshaji na kwamba fedha nyingi zitakwenda kwenye miradi ya wananchi kuliko kuwa na baraza kubwa ambalo litatumia fedha nyingi ikiwemo kugharamia magari na mafuta yake.
Hata wapinzani walipokuwa wakiomba kura kwa wananchi walikuwa wakieleza namna watakavyoweza kupunguza wizara na kuwa na mawaziri zaidi ya 15 hadi 20 lengo likiwa ni kupounguza gharaza za serikali katika kulihudumia hatua ambayo sidhani kama inahitaji mjadala mkubwa wa kufanya hivyo.
Suala la Waziri Mkuu kwa kweli anahitajika mtu ambaye ataweza kutuvusha hapa tuliopo hasa kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa uchaguzi ambapo bunge la safari hili limeweza kukusanya watu wa aina mbalimbali na wapinzani wakipata nafasi nyingi hivyo Waziri Mkuu atakuwa na nafasi yake kama msimamizi wa shughuli za unge.
Waziri Mkuu aliyepita Bw. Mizengo Pinda sio kwamba hafai kurudia kwenye nafasi yake hiyo kwasasabu ameweza kufanya kazi kwa kiasi chake na kwamba suala lake la ‘kilimo kwanza’ ambalo anatakiwa bado azidi kusimamia, lakini changamoo zilizojitokeza rais anaweza kuchagua mtu mwingine ili mambo yaende hasa kusimaia ahadi zake.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kweli watendaji katika maeneo mbalimbali wameweza kufanya kazi ya ziada kuhakikisha wanashinda uchaguzi uliopitwa maeneo mengine majimbo ya ubunge na viti vya udiwani vimechukuliwa na wapinzani hivyo, suala la waziri mkuu ni suala linalohitajika Rais afanye kazi ya ziada kumteua mtu ambaye atasafisha maeneo hayo ili kuhakikisha chama hicho mwaka 2015 kinakuwa na hoja za kujibu kwa wananchi.
Sababu ya kueleza hivyo kama nilivyoeleza huko juu ni kwamba ahadi hizi zilizotlewa na Rais kwa kweli zinahitaji kusimamiwa na Mawaziri hawa atakaowachagua vinginevyo Rais na baraza lake likishindwa kufanya kazi inayotazamiwa na wananchi na Watazania waliowengi hasa wale wa mleno wa ushoto kampeni kwa chama hicho mwaka 2015 zitakuwa ngumu mno.
Rais anatakiwa kuchagua mawaziri ambao licha ya kutekeleza ahadi zao kama waunge kwenye maimbo ao, ia watatumia nafasi hiyo kuhakikisha wanakiwekea mazingira mazuri chama hicho kutokana na namna kilivyopigwa chini katika maeneo mengi.
Kutochagua mawaziri waadilifu na wachapa kazi kitakiathiri chama hicho kwasababu hivi sasa Watanzania hawachagui chama wanaangalia mtu aliyesimamishwa.
Kwa mtazamo wangu nadhani nafasi ya Waziri Mkuu inamfaa sana Bw. Edward Lowasa, ndiye atakayefaa kurudia nafasi yake hiyo kwa kuwa anaweza kusimamia kazi zilizopo mbele yake licha ya mapungufu yaliyojitokeza ya kukutwa na kashfa ya kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond hatua ambayo aliwajibika kwa hilo.
Lowasa pamoja na kupatikana na kashfa hiyo ambayo hata Rais alisema ilikuwa ni ajali ya kisiasa na amini kwamba baada ya kukaa nje kwa kipindi chote na kuteuliwa Bw. Mizengo Pinda ambaye pia alifanya kazi nzuri, ameweza kujifunza na kujutia makosa yake hivyo kurejea tena kwenye nafasi hiyo kutamfanya aweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi na hivyo kuivusha CCM na hali iliyojitokeza kwenye uchaguzi uliopita.
Ukiondoa kashfa hiyo, lakini Bw. Lowasa amefanya kazi nzuri tu ya kusimamia shughuli za maendeleo Mawaziri walisimamia maagizo yake ya kazi zilizotolewa, walihamasisha maendeleo, Wakuu wa Mikoa, Ma-DC na Wakurugenzi wa halmashauri nao waliweza kufanya kazi sawasawa na pale Waziri Mkuu huyo alipofanya ziara za kukagua shughuli za maendeleo kila mmoja alihisi kumuogopa.
Nakumbuka alivyoweza kuzima upitishaji wa mafuta katika bandari ya Tanga ambapo wasafirishaji wengi wa mafuta walitumia mwanya wa kukosekana kwa ‘flormitter’ ya kupimia mafuta yanayoingizwa, kukwepa kulipa kodi ya serikali na hivyo kuingiza mafuta na kuikosesha serikali mamilioni ya shilingi.
Hatua hiyo, ilimfanya Bw. Lowasa kufanya ziara ya ghafla mkoani humo na kuifungia bandari hiyo isipitishe mafuta tena hadi hapo Mamlaka ya usimamizi wa bandari kwa kushirikiana na nTRA watakapofunga ‘flour mitter’ ambayo itasaidia waingizaji wa mafuta waweze kupima mafuta yao na kulika kile kiingiacho badala ya kukadiria na kupima kwa njia ya kawaida.
Mbali na kazi hiyo, zipo zingine ambazo zimeuwa na tija kubwa kwa serikali na wananchi ambazo amezifanya kabla ya kutoka kashfa hiyo ambayo hata hivyo kimsingi ilifika mahali ikaonekana kwamba tatizo hilo lilikuwa ni la kisiasa miongoni mwa wabunge huko bungeni leo hii tukishuhudia mabadiliko makubwa kabla ya baraza hilo kuchaguliwa.
Hakuna binadamu aliyekamilika Watanzania tukizidi kumhukumu na kutoa miguno itakuwa ni kumuonea kwasababu viongozi waliopo wote wamekuwa na nia njema ya nchi hii na inapotokea wanashindwa kusimamia kazi na mipango ya wananchi, wapo wanaosema hawajali maslahi ya Taifa, je ni Mtanzania gani huwa anajitambua uzalendo wake kwa Taifa lake kwa maana ya kusaidia ulipaji wa kodi na kusaidiana na wananchi wa mtaa wake kuchangia kazi za maendeleo.
Mzee wa bonde, alamsiki!

No comments:

Post a Comment