Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Saturday, November 27, 2010
SAMAKI ALIYEPOTEA MIAKA 60 ILIYOPITA ATENGEWA ENEO MAALUM KIGOMBE
WAKAZI wanaoishi katika mwambao wa pwani ya bahari ya hindi, wametakiwa kutunza rasilimali ziliozomo katika maeneo ambayo yametengwa maalum kwa ajili ya uhifadhi wa viumbe vya bahari ili kuboresha na kupanua uchumi wa wananchi licha ya kuwepo matuminzi endelevu ya rasilimali hizo.
Meneja wa Kitengo cha Hifadhi za bahari na Maeneo Tengefu, Dkt Abdilahi Chande alisema hayo kwenye ufunguzi wa mkutano wa wadau juu ya uundaji wa mpango wausimamizi wa hifadhi ya bahari ya Silikanti ya Tanga katika eneo la Kigombe ambako samaki huyo wa aina yake duniani amekuwa akipatikana hapo mara kwa mara.
Alisema hifadhi ya bahari ni muhimili mkubwa wa rasilimali zilizomo ndani yake hivyo jamii inayoishi kwewnye maeneo hayo wana wajibika kuwa walinzi wa rasilimali hizo ambazo zitaweza kusaidia vizazi vijavyo na pia kusaidia uchumi wa nchi kwa sehemu kubwa ya uhifadhi wa viumbe hiyo.
"Kama wananchi mnaoishi katika maeneo ya bahari bmnalo jukumu kubwaq la kusimamia rasilimali zilizomo ndani ya bahari kwa lengo la kuleta tija kwa maslahi ya wananchi...Usimamizi bora na shirikishi utalenga katika kupanua uchumi wa wananchi licha ya kuwepo kwa matumizi endelevu ya rasilimali hizo," alisema Dkt Chande.
Katika mkutano huo alisema malnego makuu ni ya kurejesha maoni na mawazo ambayo ya wananchi ambayo waliyatoa wakati wakifanya mikutano katika maeneo yao wanayoishi ambako waliweza kupata taarifa mbalimbali juu ya matumizi sahihi ya rasilimali, matatizo ya kiuchumi na kijamii pamoja na yale yanayoharibu mazingira ya baharini. Hivyo mkutano hio ungechambua na kupata mpango mkakati wa namna watakavyosimamia hifadhi hiyo ya Silikanti Kigombe.
Awali Kaimu Mhifadhi Mfawidhi wa Silikanti Kigombe Bw. Sylevester Kazimoto alisema kuwa serikali tayari imepitisha kwamba eneo la Kigombe liwe hifadhi tengefu kwa ajili ya samaki aina ya Silikanti ambaye alipotea duniani miaka 60 iliyopita kabla ya kuonekana tena nchini Afrika ya Kusini na baadaye kuonekana mwaka 2003 tangu atoweke katika eneo la bahari ya Kilwa mkoani Lindi.
Bw. Kazimoto alisema eneo la Mtakatifu Luciana nchini Afrika ya kusini lilitengwa kuwa eneo tengefu la samaki huyo sehemu nyingine hapa nchini ni eneo la Mafia lililotengwa mwaka 1994, ghuba Mnazi iliyopo katika maiingilio ya mto Ruvu iliyotengwa mwaka 2000 na hifadhi ya silikanti ya Kigombe iliyotengwa mwaka 2009.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment