Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Saturday, November 20, 2010

Nyumba hizi bado zipo katikati ya Jiji la Tanga

Moja ya nyumba ya makunti ambayo katika miji ya mwambao wa bahari kama hapa Tanga utaikuta ikiwa ipo katikati ya Jiji hii na nyingine chini zipo barabara ya 16 eneo la Mlango wa Chuma.
Wakazi wa nyumba za makuti ukiwakuta wenyewe wamekaa nje tena hawana wasiwasi kabisa maisha yanakwenda.
Hii ambayo pia ipo barabara 16 mlango wa chuma, kidogo mwenye nyumba hii anajaribu kuibadilisha ili angalau ifanane na nyingine ingawa bado juu kuna kuti!
 Hii pamoja na kwamba mwenye amejitahidi kupanda maua ili ipendeze lakini bado haina mvuto kutoka na jinsi ilivyo. Kwa kweli kupata nyumba bora katika Jiji la Tanga itachukua mda kutokana na wanaosimamia sheria za mipango miji hawawezi kuchukua hatua kwani wapo wanaouza nyumba za aina hiyo lakini utakuta bado watu wanajenga nyumba za chini na wanaezeka makuti wakati sheria ipo kwamba eneo lote la Ngamiani na sehemu nyingine ya Jiji hili endapo nyumba itajengwa basi ijengwe ya ghorofa walau tano na kuenelea.
Jengo hili la zamani sana katika mji wa Tanga eneo la bandari...Ni sehemu mojawapo inayovutia ingawa nyumba za makuti bado zinatufanywa watu wa Tanga tuendelee kusuasua kufikia maendeleo.

No comments:

Post a Comment