Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Saturday, November 20, 2010

Manchester yarejea kilele na kuipita Arsenal juu kwa juu

Beki wa kushoto wa timu ya Manchester United Patrick Evra akiruka juu kuandika bao la kwanza kwa kichwa kwa timu yake dakika 32 baada ya kuunganisha krosi safi kutoka winga ya kulia iliyopigwa na Ji-Sung Park na kumuacha mlinda mlango wa Wigan Ali Al Habsi asijue la kufanya. Bao hilo lilidumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili Wigan walipata pigo baada ya wachezaji wake wawili Antolin Alcaraz kutolewa nje kwa kupewa kadi nyekundu baada kumchezea rafu na refa Atkinson kumpa kadi ya pili ya njano alipomchezea rafu mbaya Luis Nani kabla ya mchezaji mwingine wa timu Hugo Rodallega naye kupewa kadi nyekundu baada ya kumrukia na miguu miwili beki wa kulia wa Manchester United Rafael.

Kocha Alex Furguson alimwingiza Waney Rooney kipindi cha pili baada ya kutoonekana uwanjani kwa kipindi cha miezi mitano kutoka na kuwa majeruhi na kusongwa na mambo mengi ya nje ya uwanja ambapo aliweza kuisaidia timu yake na Javier Hernandez 'Chicharito' alifunga bao safi kwa kichwa akiunganisha mpira wa krosi kutoka kwa Rafael. Man imefikisha pointi 28 sawa na Chelsea huku Arsenal akibaki na pointi 26.

No comments:

Post a Comment