Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Saturday, November 27, 2010

MTANGAZAJI MAHIRI SHABAN LUPA NDANI YA UPLANDS FM NJOMBE


ALIYEKUWA MTANGAZAJI WA REDIO YA MWAMBAO FM YENYE MAWIMBI YA 100.6 SHABAN LUPA AKIWA NA MTANGAZAJI MWENZAKE WA KIKE SARAH MANDE WAKIWA HEWANI KWENYE KIPINDI CHA KIJAMII.
                                   Na Mzee wa Bonde
ALIYEKUWA mtangazaji mahiri wa kipindi cha michezo cha redio ya 100.6 Mwambao FM 'Sauti ya Tanga', Shaban Lupa, amepata kazi katika kituo kipya cha redio Uplands kilichopo katika mkoa mpya wa Njombe baada ya kuondoka katika redio hiyo ya Mwambao.

Lupa ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na kuweza kuzifunika redio nyingine zilizokuwepo Jijini Tanga, ka utangazaji wake mahiri wa michezo katika anga mbalimbali hasa taarifa za kispoti za nje ambazo wanazi mbalimbali wa timu za Ligi Kuu ya Uingereza, walikuwa wakifuatilia kipindi hicho kujua timu zao zinavyoenelea ikiwemo wakati wa usajili.

Akilonga na blogu ya jamii na matukio, Lupa alisema ameamua kujikita katika mkoa huo mpya wa Njombe  kuitumikia redio hiyo mpya ambayo kesho imeandaa bonaza la kusherehekea miaka mitatu tangu kituo hicho kianzishwe mwaka 2007.

Lupa ambaye umahiri wake hautasahauliwa katika redio mahiri, yupo katika mkoa huo takribani miezi miwili sasa na tayari ameanza kuungurumisha kazi kwa ufanisi mkubwa ingawa alisema baridi imekuwa ikikwarauza sauti yake kutokana na vijimafua vinavyosababishwa na baridi kali.

No comments:

Post a Comment